Proverbs 17


1 aAfadhali kula ukoko mkavu ukiwa na amani na utulivu
kuliko kukaa kwenye nyumba ya karamu kukiwa na magomvi.


2 bMtumishi mwenye hekima atatawala juu ya mwana aaibishaye,
naye atashirikiana katika urithi kama mmoja wa hao ndugu.


3 cKalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu,
bali Bwana huujaribu moyo.


4 Mtu mwovu husikiliza midomo mibaya;
mwongo husikiliza kwa makini ulimi wa madhara.


5 dYeye anaye mdhihaki maskini huonyesha dharau kwa Muumba wake;
yeyote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa.


6 eWana wa wana ni taji la wazee,
nao wazazi ni fahari ya watoto wao.


7 fMidomo yenye uwezo wa ushawishi haimfai mpumbavu:
je, ni mibaya kiasi gani zaidi midomo ya uongo kwa mtawala!


8 gKipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho;
kokote kigeukiapo, hufanikiwa.


9 hYeye anayesamehe kosa hudumisha upendo,
bali yeyote arudiaye jambo hutenganisha marafiki wa karibu.


10 Karipio humwingia sana mtu mwenye kutambua
kuliko mapigo mia kwa mpumbavu.


11 Mtu mbaya hupenda kuasi tu;
mjumbe asiye na huruma atatumwa dhidi yake.


12 iNi afadhali ukutane na dubu aliyenyang’anywa watoto wake,
kuliko mpumbavu katika upumbavu wake.


13 jIkiwa mtu atalipa baya kwa jema,
kamwe ubaya hautaondoka katika nyumba yake.


14 kKuanzisha ugomvi ni kama kutoboa bwawa la maji;
kwa hiyo acha jambo hilo kabla mabishano hayajaanza.


15 lYeye asemaye kuwa asiye na haki ana haki,
naye asemaye kuwa mwenye haki hana haki:
Bwana huwachukia sana wote wawili.


16 mFedha ina faida gani mikononi mwa mpumbavu,
wakati yeye hana haja ya kupata hekima?


17 nRafiki hupenda wakati wote
naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida.


18 oMtu mjinga hupana mkono ili kuweka rehani,
naye huweka dhamana kwa jirani yake.


19 Yeye apendaye ugomvi apenda dhambi;
naye ainuaye sana lango lake
Kuinua lango maana yake ni kusema kwa majivuno.
hutafuta uharibifu.


20 Mtu mwenye moyo mpotovu hawezi kufanikiwa;
naye ambaye ulimi wake ni mdanganyifu huanguka kwenye taabu.


21 qKuwa na mwana mpumbavu huleta huzuni;
hakuna furaha kwa baba wa mpumbavu.


22 rMoyo wenye furaha ni dawa nzuri,
bali roho iliyopondeka hukausha mifupa.


23 sMtu mwovu hukubali rushwa kwa siri
ili kupotosha njia ya haki.


24 tMtu wa ufahamu huitazama hekima,
lakini macho ya mpumbavu huhangaika
hadi kwenye miisho ya dunia.


25 uMwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake
na uchungu kwa yeye aliyemzaa.


26 vSi vizuri kumwadhibu mtu asiye na hatia,
au kuwapiga sana maafisa kwa ajili ya uadilifu wao.


27 wMtu mwenye maarifa hutumia maneno kwa kujizuia,
naye mtu mwenye ufahamu ana moyo wa utulivu.


28 xHata mtu mpumbavu hudhaniwa kuwa na hekima kama akinyamaza,
na mwenye ufahamu kama akiuzuia ulimi wake.
Copyright information for SwhKC